“Mimi ni msaniix2
Kioo cha jamii (kioochajamii)
Mimi naona mbali x2
Kwa darubini kali (kwa darubinikali)”
Nibaadhi ya maneno katika wimbowa ‘Darubini Kali’ ulioimbwa na msani iAfande Sele
Takribani miaka mitano iliyopita. Kipande hicho kina zungumzia sanaa na jamii, namna
Vitu hivyo viwili vinayotegemeana.

Fasihi ni kioo cha jamii. Sanaa ni picha ya jamii iliyokuwepo tangu enzi za kale ikionesha mambo yaliyomo katika jamii
Kwa udogo na mapana yake kama ilivyo darubini. Utamaduni ni sehemu yamaisha,
Ni mambo ambayo huanzia kwetu wanajamii, ni asili au utambulisho wa jamii nyingi.
Hapo mwanzo sanaa ilikuwa kiungo muhimu cha kuenzi na kuthamini tamaduni za jamii
zetu,na tamaduni hizo zilipendwamno na watu wote wakiwemo vijana. Lakini sasa,
kutokana na mwingiliano wa kijamii, tamaduni nazo zikaanza kuchuja na mpaka sasa
tunashuhudia upotevu wa tamaduni zetu hususani sanaa za asili kama vile muziki,
maigizo, ngonjera, ushairi kutokana na teknolojia ya utandawazi.

Kwa kuona hilo, shirika lisilo la kiserikali“Tanzania Youth Culture Exchange Network’’
(TYCEN) linayohusu vijana na utamaduni liliandaa mradi unaoitwa ‘SambaaSanaa’
Ulio anzishwa Februari, 2017. Mradi huu ulilenga vijana kati ya miaka15-35, ikifadhiliwa na Royal Danish Embassy, jijini Dar es Salaaam.
Muasisi wa Shirika hili, Bw.Chris Ndallo alisema kuwa lengo ni kuinua vipaji vipya vya
Kitamaduni na kuwapa fursa ya kuonesha vipaji hivyo ili waweze kujiajiri kupitia sanaa
Za utamaduni, kitu ambacho kitawawezesha kujikwamua na tatizo la ajira linalowakabili
Vijana wengi nchini.

Sambaa Sanaa ilijikita zaidi katika mfumo wa kutoa semina pamoja na vijana kukaa
kambini ambapo watajengewa uwezo wa kuonesha vipaji vyao. Washiriki walitapata nafasi ya kushiriki katika tamasha la kimataifa (Bagamoyo International Festival of Art and Cultural.
Mafunzo mengine yaliyotolewa kwa vijana ni jinsi ya kuendesha taasisi za
Kitamaduni, namna ya kutumia fursa zinazowazunguka na kutengeneza fursa bunifu za
Sanaa na kitamaduni.

“Idadi kubwa ya wanasanaa wa kitamaduni wanakosa usimamizi mzuri wa kazi zao,
Masoko na namna ya kujitangaza, suala ambalo hupelekea kazi zao kutotambulika na
Badae kufakabisaaaa kwa vikundi vya kitamaduni” alisema Bw.Ndallo.
Vya kale ni dhahabu. Pamoja na kwamba tunakwenda na wakati, mjasiri hapaswi kuacha asili. Wakati tukiendelea kuonekana watumwa wa utandawazi, angalau tujitahidi kurudisha ile hadhi na nafasi ya Tamaduni zetu, tuvipende vya kwetu.

Agness Kimwaga, Afisa habari mkuu wa Baraza la Sanaala Taifa (BASATA) alisema
Kuwa kutokana na utandawazi tamaduni zetu zimepoteza uhalisia, hakuna nafasi tena
Ya vijana kusikiliza hadithi za kitamaduni kutoka kwa wazee wetu, matumizi ya vifaa vya technolojia vimechukua nafasi kubwa kwa vijana. Aliongeza kuwa, masomo ya sanaa na utamaduni yatiliwe mkazo katika madarasa ya msingi.
Nae mkurugenzi wa ukuzaji sanaa na masoko Bi.Viviani Shalua kutoka BASATA
alizungumzia ushiriki wa vijana katika sanaa kuwa unaridhisha, vijana wengi
wanashiriki katika michezo ya sarakasi, muziki, uchoraji, na ubunifu wa mavazi. Baraza
lipo bega kwa bega kuwalea wasanii na kuhakikisha wanafanyakazi kwa kufuata
misingi na taratibu zilizowekwa na baraza hilo.

Aliongeza kwa kusema, teknolojia inasaidia kama itatumika vizuri. Kazi mbalimbali za
Sanaa zameweza kujulikana nje ya nchi, na wasanii kujulikana kutokana na matumizi
Mazuri ya mitandao ya kijamii hususani Instagram. “Napenda kutoa wito kwa serikali
Waendelee kushiriki kikamilifu kuitetea sanaa nchini kwani Taifa bila sanaa ni kama
gogo”AlisemaMkurugenzi.

Mtaalam wasanaa za jukwaani Bw.Chedieli Senzighe amesema kuwa miongoni mwa
sektayenyeushirikiwavijanawenginisanaakwasababunirahisi,wawezaifanyiakazi
hatabila kusomea. Pia ameeleza kuwa kuna fani tofauti tofauti kama vile uigizaji
uimbaji, ngoma, ususi, na sanaa zote hizo ni tamaduni, hivyo anawahasa vijana waleo
kutopotosha ladha ya jamii kwa kuchanganya na sanaa za mataifa mengine.

TYCE lilianzishwa mnamo tarehe 24/7/2009, na makao yake makuu ni Dar es Salaam,
Tanzania. Kupitia kaulimbiu ya TYCEN “Vijana, Mabadiliko na Maendeleo Endelevu”,
Sambaa sanaa imehakikisha vijana wanapata fursa, na sanaa inarejea kwa
Kishindo katikati ya jamii ya sayansi na technolojia.

Imeandaliwa na Jonetha Peter kukota TYCEN.
#pen4Apen campaign
Tycen on Facebook
Tycen on Twitter
All rights reserved Tanzania Youth Cultural Exchange Network (TYCEN) | Developed by EDUMEK